Friday, July 24, 2009

Shida ya kupendwa kiasi hicho?

Nasikia wakina dada wanatumia madawa ya sumu ili kuongoza makalio na mahipsi (Bust up au Lift up cream) – eti ili wapapatikiwe na sisi wanaume. Sijapata kuona ujinga wa namna hiyo. Siyo tu ugonjwa, bali ni wenda wazimu Fulani.

Hii inakuja siku chache baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kutoa athari zinazoweza kutokea kwa madada wanaotumia masumu hayo, ambayo yanaendelea kuuzwa na baadhai ya maduka hapa nchini.

TFDA imetangaza kwamba dawa hizo zina madhara kwa binandamu na kwamba zinasababisha saratani ya ngozi , magonjwa ya figo na hata magonjwa ya ubongo katika kipindi cha maisha ya mtumiaji.

Inasemakana watumiaji kwa sasa ni wasichana, hasa wanafunzi wa vyuo, sekondari na mabinti wa mitaani wenye tamaa ya kubadilisha maumbo kwa lengo la kuwavutia wanaume.

Inashangaza kweli. Hivi nani kawaambia hawa madada, wanaohaha kupata wanaume, kuwa wanaume wote wanapenda wanawake wenye mitako mikubwa kama nyumba na mihipsi inayoning’inia kwenye miili yao?

Kuna wengine wanapenda vipotable na kwa vyo vyote vile kila mtu ana kitu chake kinachomvutia kwa demu wake au fala lake (ndivyo wanaume wanavyoitwa).

Makalio? Mahipsi? Mimi inanikumbusha mzigo wa lori la tani kumi na kujaribu kuupakia kwenye gari la tani tatu na nusu. Utavunja springi!

Soko la wanaume ni kubwa sana. Kuna wengine wanaopapatikia hivi na wengine vile. Na kuna sisi tusiopapatikia wanawake wakubwa kama nyumba.

Lakini pia kuna wanaume wanaopenda wachumba wakubwa kama kasri. Wanawake nao ni vile vile katika kuvutiwa na wanaume – haidhuru wanaume wengi wanaapa kuwa hawitaji kunywa nasumu ili kuvutia wanawake. Wanasema kuvutio cha kwanza cha wanaume ni pochi yake tu.

Labda kweli. Kwa nini wanaume wanaitwa ATM au buzi au ‘mnene’? Sina uhakika. Lakini la kutisha ni kitendo cha mtu kunywa masumu na kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kupata wanaume! Wakina dada, hata mseme nini, nadhani mnawapa vichwa sana wanaume. Mpaka kufikia kutaka kujiua kwa makusudi mazima?

Kwa upande mwingine TFDA nao wanahitajiwa kulaaniwa vikali. Mbona kila siku tunaambiwa masumu hayo yanaingizwa nchini na kuuzwa wazi wazi katika baadhi ya maduka hapa nchini? Cha kushangaza ni kuwa sisi wananchi hatujaona hata siku moja waalifu hao waotawanya na kuuza madawa hao kuchukuliwa hatua za kusheria.

Vyombo vya dola vinasema kuwa vinawajua wahalifu waoshughulika na mihadharati na madawa ya sumu. Lakini hata siku moja hutasikia kuwa wamekamatwa watu wnaouza masumu hayo. Kuna nini?

Au ndiyo tabia yetu ya karibu kila sehemu nchini. Watawala wanavunga kuwa wanalifanyia kazi tatizo za rushwa nchini. Lakini tunazidi kunaona magendo na vitu haramu vikiingizwa nchini kinyume cha sheria. Wanaotenda makosa hayo hatuwaoni mahakamani hata siku moja!

No comments: