Monday, September 21, 2009

Chombezo la Adam Lusekelo

Nilikuwa nasikia mambo ya kutisha kuhusu ushirikina. Kuwa watu wanaenda kiwango kisichofikirika, ili kufikia malengo yao katika maisha. Wengi wanaenda kuloga.

Wanawake wengi wanaenda kuloga ili wapate wachumba. Wakimpata mchumba wanaenda kuloga ili mchimba asimwache. Nimeongea na wanaume wengi kwenye migahawa ambao wamekiri kuwa ndoa zao zimevunjika baada ya mzee kukuta tunguli zikining’inia chini ya kitanda cha maharusi. Nasikia wanawake wanapenda kuloga penzi, kusudi liwe moto moto na njemba isiangalie pembeni.

Wanaume wanaloga sana kupata vyeo. Sasa hivi wengi wa wanasiasa wetu wanalogana ili kushinda kwenye ubunge. Nasikia wakati wa kampeni za uchaguzi jamaa wanakuwa na ‘kamati ya ufundi’ ili kuloga watokeze washindi katika uchaguzi.

Unajua saikologia ya ulozi siyo ngumu sana. Wachawi wanaitumia kuweza kushitua akili zako, ili uweze kuamini kisichoaminika. Sasa kama akili yako itaamini kwa dhati kuwa ulozi huo utafanya kazi basi utajikuta kuwa kweli mambo yanaenda kama unavyotaka.

Mwaka 1905 mpaka 1907 wafuasi wa Kinjeketile waliambiwa na mchawi wao kuwa risasi za wakoloni wa Kijerumani zitakuwa maji, katika mapigano ikiwa watapiga ukulele ‘Maji! Maji! wakati risasi za Wajerumani zikirushwa katika vita hiyo ya ukombozi. Kwa hiyo wakathubutu.

Huo ushupavu haukutosheleza sana. Kwani silaha za wananchi hazikuwa bora. Katika mapambano unahitaji silaha zenye kufaa juu ya kuwa na ushupavu na nia ya kushinda.

Wapiganaji wa Mau Mau, nchini Kenya walikuwa wanakula kiapo cha ubongo wa msaliti aliyechinjwa mbele yao. Ubongo huo ulichanganywa na damu na kuliwa na makuruta wa Mau Mau huku wakiapa kuwa watamdunda Mwingereza na kuikomboa nchi yao.

Kuna limbwata. Mdada anaambiwa aweke kipande cha nyama sehemu zake za siri, halafu ampikie mpenzi wake. Akimlisha tu, basi jamaa ataharibikiwa. Na kweli akili ya yule mwanamke itashitushwa sana kumuona mpenzi wake anakula uchafu huo. Amethubutu na ataamini kuwa kuanzia wakati huo njemba hafurukuti.

Mwana siasa anaweza kupelekwa makabirini saa sita usiku na kukubali kunyolewa sehemu za siri ili ashinde. Kwa wanaume anaambiwa ukifanya kitu kisichofikirika, utakiwa tajiri wa kupindukia. Lakini wendawazimu wanaamini hiyo. Ndiyo maana unasikia mambo ya ajabu yakitokea katgika ushirikina.

Hivi sasa polisi mkoani Rukwa, wanamshikilia Afisa tabibu wa Hospitali ya Nkasi, kwa tuhuma ya kumnajisi mtotoo wake wa kike wa umri wa miaka mitano.

Inasemekana kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa Agosti 29 mwaka huu, nyumbani kwa mtuhumiwa katika eneo la Isunta. Binti yake alipiga makelele kwa maumivu na majirani walikuja kumkamata na kumpeleka kituo cha polisi cha Namanyere.

Chizi huyo alivyoulizwa akasema kuwa alikuwa amelewa! Mimi nashangaa hata walimuuliza wa nini. Wangemkata kajambazi kake kanakomnning’inia hapo chini kwa sababu naona kalinfamya awe kichaa kabisa!

Nahisi sababu hasa ya kufanya kitendo hicho cha uovu ni kuwa mchawi wake alimpa masharti ya kupata utajiri. Tumesikia manbo mingi sana yasiyofikirika ambayo vichaa hao wanavifanya ili kupata eti utajiri. Wanaume wanaambiwa wawaue au wawabake mama zao wazazi, au watoto wao.

Mimi naona adhabu ya kifungo haitoshi. Tuanze kufikiria adhabu ya pale pale. Jamaa kama hawa wahasiwe. Siyo watu hawa. Kwani wala hata wanyama hawabaki watoto wao. Hio ni ugonjwa, na dawa yake ni kutoa hiyo sehemu inayoleta ugonjwa huo. Kama tunavyotoa jipu mwilini!

1 comment:

Anonymous said...

Yes I agree with you bro Adam that Kanumba should take this as a challenge. British Concil will help him to improve his language.

But if you look more deeper this is not Kanumba's fault it is the whole system of education in TZ. Fine Kiswahili is our National language but when it come for international matters what language should I speak? That is why during the interviews we TZ do not get good jobs bicoz we can not express ourselves. we remain saying I mean nanii, naniii!