Saturday, November 21, 2009

Si ujana au uzee, ni uadilifu!

Wala tusijidanganye kuwa tukia na watawala vijana ndiyo mambo yatakuwa safi kabisa Tanzania. Akizungumza na njini Dar es Salaam na vijana kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakishiriki katika mpango wa kulea Uongozi wa Afrika (African Leadership Initiative) Rais Kikwete alisema kuwa vijana ndiyo Tanzania ya kesho na kama haikuweza kuwawekeza vya kutosha katika vijana wao na maendeleo yao, basi itakuwa haiwezi katika hali yake ya baadaye.

Rais Kikwete aliondoa kusikia kwa wachambuzi wa habai kama ataendelea na urais au hapana. Inaonekana ataendelea. Amesema akiendelea basi atawachngamkia vijana katika uongozi nchini.

Nakubali. Na maneno haya niliyasikia zamani sana – kuwa eti sisi ni taifa la kesho, eti sisi na tegemeo la nchi yetu tukufu Tanzania. Lakini rika langu limeangalia na kutafakari na kuona mambo yanavyokwenda na tukagundua kuwa yote hayo yalikuwa danganya toto.

Hapa tunazungumzia kuhusu madaraka. Na kitu madaraka ni simi inayokata pande zote mbili. Ni kali sana. Ukichukua vijana, mimi naona, ukimwondoa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Mzee Rashid Kawawa, Mzee Abdul Sykes na wengine wachache wasiofika kumi, watu hawa waliochukua madaraka ujanani, ni wachache sana waliobaki kuwa ‘watu wa kawaida’.

Nilibahatika kuwaona wote kwa karibu sana wakati mimi nilivyokuwa kadogo. Mpaka walivyostahafu walikuwa wako vile vile, ila umri ndiyo ulionyesha, siyo kwa kusem hovyo, bali kwa busara zao.

Leo uzao wetu umeanza kunyemelea uzeeni. Wenzetu wengine wamepata madaraka makubwa sana. Lakini mimi nawaona wale wale. Wengine hawna taabu, lakini wengine wamekuwa vichaa kabisa. Wamelewa madaraka kabisa! Mpaka imefikia kuwa leo ukiwaona mafree wa Pugu unawakimbia kwa aibu.

Nikaanza kuwauliza wenzangu – hivi kwa nini wale wanamapinduzi tuliokuwa nao shule, tukaapa kufa kuikomboa Tanzania wamebadilika manna hiyo? Kwa ujumla tukagundua kuwa wengi wenye majidai ya kitoto na kijinga walikuwa wametokea kwenye kwenye nyumba za tembe kule kwao. Wametokea kwenye umasikini wa kutisha. Aliyepafanya mpaka waone shule alikuwa ni Baba wa Taifa na siasa yake ya elimu kwa wote. Hivi hivi wangekuwa wanachunga mbuzi kwao tu.

Kwa hiyo vijana hao, ambao sasa wamekuwa madarakani wanadiriki hata kumponda Mwalimu, kwa kuwawezesha kusoma shule na sasa wanataka kuwa viongozi. Kwa babau za kisaikologia baado wanaukimbia ule umasikini waliokuwa nao kabla hawajakuwa wamekombolewa na limu hiyo.

Kwa hiyo nyumba moja haitoshia, bali nyumba nane. Gari moja halitoshi ila magari kumi. Watoto kusoma Tanzania haiwezekani ni Ulaya. Mabinti zao wakipata chunusi puani, hakuma hospitali Tanzania, mpaka aende ulaya au sausi. Huo unaitwa ulimbukeni na siku hizi utauona sana kwa hao wanaoitwa vijana.

Na kijana ni kijana. Anataka wanawake wote wawe wake, ukimtaka mmoja utafukuzwa kazi. Majina mengi ninayo ya uhuni wanaofawanya hao wanaoitwa vijana wanaowaonea wenzao kwa mambo ya kupuuzi. Njemba imeshindwa kubonga, basi inaondoa upinzani kwa kumfukuza kazi mwenzake anayeshinda.

Kazi hawezi, lakini kwa sababu ni mtoto wa fulani, basi anaendelea kumbandikwa katika cheo hicho. Naona wengine wananing’inia kwa majina ya baba zao. Kwani Mwalimu na Mzee Kawawa walitegemea majina ya Baba zao?

Uchizi huo ukiendelea Africa itaanza kutawaliwa na watoto wa marais wa sasa. Usultani umeanza Gabon, Misri, Mzee Museveni nae anataka kufanya maajabu huko Uganda.

Tunachotaka ni viongozi wenye busara, siyo uzee au ujana. Kuna wazee wahuni na utawaambia vile vile. Na kuna vijana, na wao ndiyo wanaweza kuwa waharibifu zaidi. Nao tutawazomea vile vile.
Kwani hivi sasa, Tanzania inaburuzwa na matapeli walichache wenye hela ambao wanataka kuteka nyara nchi yetu. Ni wazee wale? Si vijana majambazi, wenye vijisenti tu, ambao wamekinunua chama tawala?

1 comment:

Anonymous said...

Nimependa sana hiyo analysis yako ya tamaa ya viongozi kujilimbikizia mali hata kama wanayo ya kutosha. Ni asili ya umaskini uliokithiri huko walikotoka, na hata sasa ingawa wana mali ya kutosha, akili yao inawatuma tu kulimbikiza. Hata hivyo hiyo sio excuse ya kuwaibia wananchi na kukosa uadikifu. Imabidi wawajibishwe.
Teacher.